Binti wa miaka 15 acharangwa na visu kisa wivu

Binti mdogo wa miaka 15 raia wa Argentina Julia Alvarez amepatwa na majanga yaliyomfanya apoteze muonekano wake mzuri baada ya mabinti wawili wenye wivu kumcharanga uso wake kwa visu kisa uzuri wake uliopitiliza!
Julia anasema alikuwa anatembea kurudi nyumbani akitokea mji wa Juan Domingo Peron huko northern Argentinian ndipo wasichana hao wawili mmoja ana miaka 18 na mwingine 16 walipomvaa bila huruma. 
"Kila mtu anasema wewe ni mzuri sana..huwezi kuonekena mzuri tena tukishamalizana na wewe hapa..na watu watakuita majina mabaya'' Julia alisema haya ni maneno aliyoambiwa kabla ya kucharangwa visu usoni. 



Hili ni eneo ambalo tukio hilo la kikatili lilipofanyika .
Kupitia ukurasa wa facebook dada wa Julia aliandika ;
"Walikuwa wanamuonea wivu sana mdogo wangu na kila mara wamekuwa wakimsumbua lakini sikutegemea kama wangefika mbali kiasi hiki. Nimejaribu kuwa imara lakini kila muda naomuona mdogo wangu nataka kudondosha machozii...wamemuharibia maisha. Anasema anataka kujiua kwa sababu kila akijitizama kwenye kioo anajiona mbaya sana sasa, wameharibu familia yetu''

Polisi waliwatia mbarioni mabinti hao lakini walimuachia wa miaka 16 kutokana na umri wake ila wa miaka 18 bado wamemshikilia.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top