Ama kweli dunia uwanja wa fujo! Biharusi mtarajiwa mjini hapa, Sofia Majid amejikuta akiangua kilio baada ya kundi la wasichana watatu la jijini Dar es Salaam almaarufu Welawela kumwaga radhi kwenye sherehe ya ‘kitchen party’ yake.
Kitendo hicho, pamoja na burudani waliyoitoa vilimfanya biharusi kushindwa kujizuia na kuangua kilio kweupe.
Tukio hilo lililoshuhudiwa na The Biggest IQ, lilijiri kwenye Ukumbi wa Nashera mjini hapa hivi karibuni mbele ya Mbunge wa Viti Maalum Vijana CCM, Mkoa wa Arusha Mhe. Catherine Magige.
Welawela, wakiwa na mwimbaji wa taarabu aliyealikwa kutumbuiza,Afua Suleiman walipopewa nafasi ya kutumbuiza na ‘emsii’ wa shughuli hiyo, Hawa Chamng’anda walivamia kitanda cha zawadi cha biharusi na kuanza kucheza Makhirikhiri kwa kugaragazana kwa staili ya tendo la ndoa na kukiacha kitanda hicho kikiwa hakitamaniki kwa kukifinyanga.
Post a Comment