Mwanamke akamatwa na polisi akiwa ameficha madawa ya kulevya kunako matiti...



Kila siku wauzaji wa dawa za kulevya wamekuwa wakibuni njia mpya ya kusafirisha dawa hizo kwa nchi ambazo zimepiga marufuku usafirishaji na utumiaji wa dawa hizo.

Mwanamke mmoja Uingereza amekamatwa baada ya kukutwa akiwa amebeba dawa za kulevya aina ya Cocaine ndani ya sidiria.


Mwanamke huyo Nola Williams alikamatwa katika uwanja wa ndege wa Gatwick, akitokea Jamaica akiwa na mtoto mdogo pamoja na kijana anaejihusisha na biashara hiyo ambaye jina lake ni Raymond Goodison, ambao walikamatwa walipotaka kupanda treni kutoka uwanja wa ndege wa Gatwick kuelekea Victoria ndani ya London.

Wakati  Polisi wakifanya ukaguzi waligundua kilo moja ya cocaine yenye thamani ya dola £180,000 zikiwa imeshonewa kwenye sidiria ya mwanamke huyo.
Nola anasubiri kifungo chake, huku kijana aliyeambatana naye amehukumiwa kifungo cha miaka 13 kwa kosa la kujaribu kuingiza zaidi ya kilo moja ya dawa za kulevya aina ya Cocaine huku ikibainika kuwa sio tukio lake la mara ya kwanza.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top