Madereva wa bodaboda Singida wagoma na kufunga barabara kuu itokayo Dodoma hadi Mwanza

Waendesha pikipiki maarufu kwa jina la bodaboda na bajaji zaidi ya mianne wamefunga barabara kuu itokayo Dodoma hadi Mwanza kwa zaidi ya saa moja, kwa madai kuwa mwenzao ambaye ana hali mbaya baada ya kupigwa na kitu kizito kichwani na askari wa jeshi la polisi baada ya kugongana.

Wakitoa malalamiko yao na baadaye kufanya maandamano hadi ofisi ya mkuu wa jeshi la polisi wamesema baada ya mwenzao kupigwa hakuna hatua zozote zimechukuliwa na jeshi hilo.

Kutokana na usumbufu wa kuzuia magari na kuwazuwia baadhi yao ambao walikuwa wakifanya biashara ya kupeleka abiria jeshi la polisi baada ya kuwaomba kufungua barabara na kukaidi amri hiyo liliamua kutumina nguvu kwa kupiga mabomu ya machozi na kufanikiwa kuwatawanya huku wengine wakishikiliwa.

Kwa upande wake daktari wa mkoa wa Singida, Daktari Geofry Mgeta amesema kuwa hakuna mgonjwa aliye fikishwa hospitalini  akiwa majeruhi kwa kupigwa na chuma la kufungulia matairi na kupatiwa rufaa ya matibabu nje ya mkoa isipokuwa wana wagonjwa madereva wawili wa bodaboda walio pigwa na kutaka kuchinjwa wakati wakitaka kuporwa pikipiki zao.

Akiongea kwa njia ya simu kamanda wa jeshi la polisi mkoani Singida Thobiasi Sedoyeka amekiri kuwepo kwa tukio hilo na kusema kuwa askari wa jeshi la polisi aliyegongana na pikipiki, wakati wanafanya utaratibu wa kisheria ndipo vurugu zilipoanza na madereva wa bodaboda walitaka kuchoma moto gari lake nayeye kuamua kujilinda kwa kuchukuwa spana ya kufungulia tairi na kumpiganayo dereva wa bodaboda.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top