OMG... Baba aua binti yake na kumzika nyumbani kwake

JESHI la Polisi Mkoa wa Kagera, linamshikilia Gerald Paulo (34) kwa kosa la kumpiga binti yake, Anisia Gerald (14), sehemu mbalimbali za mwili wake na kumyonga kwa kutumia kanga.

Akizungumzia tukio hilo mjini hapa juzi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera,  Henry Mwaibambe, alisema tukio hilo lilitokea Mei 7, mwaka huu katika Kijiji cha Rugazi Kyaitoke kisha alichimba kaburi nyuma ya nyumba yake na kumzika.

Alisema walipata taarifa kutoka kwa jirani ya Paulo kuwa ameua binti yake na walipofuatilia walibaini ni kweli.


Alisema baada ya polisi kufukua kaburi hilo walikuta mwili wa binti huyo ukiwa na majeraha sehemu mbalimbali za mwili wake na kipande cha kanga shingoni.

“Kwa taarifa nilizonazo, Gerald si mara ya kwanza kufanya mauaji kama hayo, maana miaka mitano iliyopita aliwahi kuua mtu na kukimbilia Karagwe kwa jinsi hiyo hiyo, kwa tukio hili lazima sheria zichukue mkondo wake,” alisema Mwaibambe.

1 comments:

Kweli kabisa Mr. Danny ubinadamu hakuna kabisa siku hizi watu wanauana na kufanyiana matendo ya ajabu na kinyama bila hata kuwa na hofu ya Mungu

Reply

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top