Taadhari kwa picha hizi..Mauaji ya kutisha Bukoba, Wawili wauliwa na kutolewa pua

Kijana Joseph Gabriel anayefanya vibarua mbalimbali vya kujiingizia kipato amekutwa amekufa baada ya kukatwa na kitu chenye ncha kali na huku sehemu ya pua ikiwa imeondolewa sambamba na sehemu ya shavu lake la kushoto.

Mauaji haya ya kutisha yametokea katika maeneo ya kata Karabagaine katika kijiji cha Kitwe.Polisi pia walichelewa kufika eneo la tukio kutokana na kuwa katika eneo jingine ambako pia kulikuwa na tukio jingine la kutisha kama hili lilitokea siku moja kabla ya hili.


Mwanamke mmoja ambaye jina halikuweza kufahamika mara moja, amekutwa amekufa kwa kuchinjwa shingo na pua yake kuondolewa.Pua yake ilipatikana baadae karibu na eneo la tukio.Mama huyu amekutwa na mauti katika mtaa wa Kibeta kata ya Kibeta ambapo baadaye polisi waliweza kufika na kuchukua mwili wa marehemu.


Mwezi uliopita, polisi Kagera ilitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu mauaji ya manispaa ya Bukoba, ikieleza kuwashikilia watu kadhaa na kinara wa mauaji hayo, ambao majina yamehifadhiwa kwasababu za kiusalama, huku ikisema kuwa watu wawili waliuawa na polisi kwa kupigwa risasi, wakati wakiwapeleka kwenye maeneo wanakopangia uhalifu huko Bugabo halmashauri ya Bukoba.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top