Ajali!! Basi lagongana na lori mkoani Tabora

Abiria zaidi ya alobaini wamenusurika kifo baada ya basi walilokuwa wakisafiria kutoka mjini Tabora kuelekea kata ya Goweko wilayani Uyui mkoani humo kuligonga gali la mizigo katika njia panda, katika kile kilichodaiwa kuwa, dreva wa basi hilo hakuwa na breki ya kumsaidia kuchukua tahadhali ya kuepuka ajali.

Wakizungumza nasi abiria waliokuwa katika basi hilo aina ya Scania la kampuni ya Ladak lenye namba za usajili T 918 ACG,  wamesema kuwa, kutokana na mwendo wa gali hilo dreva ambaye hakujulikana jina lake mara moja, alishindwa kulimudu matokeo yakawa ni kulivaa gali hilo la mizigo aina ya Scania lenye namba za usajili T 699 ABN.

Ajali hiyo iliyohusisha magali matatu huku gali dogo likigongwa nyuma na basi hilo madreva wa magali yaliohusishwa na ajali hiyo wamewalalamikia dreva wa magali kutochukua tahadhali wanapokuwa katika matumizi ya barabara jambo ambalo litaepusha madhara ya ajali.

Akizungumza kwa njia ya simu mkuu wa usalama barabarani mkoani Tabora mratibu wa polisi Bw. Michael Dereli ajali ya basi hilo haikuwa na madhara kwa abilia, lakini katika wiki hii ya usalama barabarani watahakikisha wanatatua changamoto ya magali kama hayo ambayo hayakidhi matakwa ya kusafirisha abiria.

credits:itv habari

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top