Wagombea ubunge zaidi ya 200 wa chama cha ACT Wazalendo wapewa mafunzo maalumu...

Chama cha ACT-Wazalendo kimeendesha mafunzo kwa wagombea kwa wagombea ubunge zaidi ya 219 kwa tiketi ya chama hicho ili kuwajenga uwezo wa kampeni na uongozi pamoja na kuwa na mitazamo inayolingana kwa wagombea wote kutoka ngazi ya ubunge, udiwani na urais.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ufunguzi wa mkutano huo, kiongozi wa chama Bwana Zitto Kabwe amesema chama cha ACT kimefanikiwa kuweka wagombea 219 katika majimbo 265 ya jamhuri ya muungano na kukifanya kuwa chama cha pili kuwa idadi kubwa ya wagombea na kulazimika kuendesha mafunzo kuwajengea uwezo wa kunadi sera, pamoja kuzungumzia mambo ya kitaifa, matatizo ya jamii badala ya malumbano kama yanayoendeshwa na vyama vingine. 
Bwana Zitto amevilalamikia baadhi ya vyama vya upinzani kuanza kufanya vurugu na kuwawekea pingamizi na kuwakatia rufaa baadhi ya wagombea ubunge wa ACT-Wazalendo bila ya kuwa na sababu za msingi jambo linalochangia kupunguza kasi ya kufanyakampeni kwa wagombea, pamoja na kuwapotezea.

Aidha Bwana Zitto amesema chama hicho kitazindua kampeni ya uchaguzi mkuu katika viwanja vya Zakhiem Mbagala Agosto 30 mwaka huu na kuanza kuzunguka mikoani kueneza sera, mikakati ya chama pamoja na mpango ya maendeleo iwapo wananchi watakipa ridhaa chama cha ACT Wazalendo kushika dola.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top