Kijana Kasendeka
 ambaye alipata ajali iliyohusisha pikipiki mbili maarufu kama bodaboda 
eneo ilipo Club Royal karibu na lango kuu la kuingilia Chuo Cha Utumishi
 cha Tabora zamani kikifaahamika kama UHAZILI.
Kamera ya
 mtandao huu imelimulika tukio baya la ajari iliyohusisha pikipiki mbili
 eneo la Club Royal karibu na lango la kuingilia chuo cha Utumishi wa 
Umma cha Tabora zamani UHAZILI.
Mfuatiliaji
 wa tukio alibainisha dereva mmoja alikuwa anatokwa na harufu ya pombe 
kitu kilichodhihirisha kuwa alikuwa amelewa huku kamchukua abiria na 
akiendesha chombo cha moto.
Mashuhuda
 waliuambia mtandao huu kuwa wanalalamikia jeshi la polisi kuto 
kujitokeza mapema eneo la tukio licha ya kuwa hapana umbali unaozidi 
mita 100 kutoka eneo la tukio, mfuatiliaji wa tukio aliwahoji kama kuna 
yeyote aliyetoa taarifa kituoni dhidi ya tukio hilo lakini hakupata 
majibu.
   
Kasendeka
 akiwa anazinduka ziduka, akili inakuja baada ya kuzimia kwa muda kidogo
 kufuatia ajali iliyohusisha pikipiki mbili eneo la Club Royal karibu na
 lango/ geti la kuingilia Chuo Cha Utumishi wa Umma zamani UHAZILI.

   
Abiria na
 mhanga wa ajali hiyo akiwa anaugulia maumivu baada ya ajali iliyotokea 
muda mfupi maeneo ya Club Royal karibu na geti kuu la kuingilia Chuo Cha
 Utumishi wa Umma zamani UHAZILI

   
Mashuhuda wa tukio la ajali iliyohusisha pikipiki mbili maeneo ya Club Royal
   
Kasendeka akiwa anaangalia pikipiki yake baada ya ajali hiyo muda mfupi alipozinduka.
   
Askari wa
 Jeshi la usalama barabarani akijongea eneo la tukio. Inakadiriwa ni 
zaidi ya dakika 15 au zaidi (Kwa mujibu wa mashuhuda) zilipita ndipo 
askari alijitokeza eneo la tukio licha ya tukio hilo kutokea umbali wa 
mita za makadirio zisizozidi 100 kutoka kituo kukuu cha Polisi mjini 
Tabora.
   
Askari akifuatilia tukio hilo baada ya dakika zinazokadiriwa na mashuhuda wa tukio kuwa ni zaidi ya 15 toka ajari imetokea.
   
Askari 
akimhoji Kasendeka kabla ya kwenda naye kituoni huku mhanga mmojawapo 
kuwa tayari alishakimbia eneo la tukio na kuisaliti pikipiki eneo la 
tukio.


Post a Comment