Mgombea
wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa
Ifakara wilayani Kilombero kwenye mkutano wa kampeni za CCM ambapo
aliwaambia wananchi hao kuwa wakati wake utakuwa wa kiutendaji zaidi ili
kufanikisha maendeleo ya haraka kwa nchi na wananchi kwa jumla.
PICHA NA MICHUZI JR-KILOMBERO.
Wananchi
wa mji wa Ifakara waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa kampeni za
CCM ndani ya uwanja wa saba saba wilayani Kilombero,wakimshangilia kwa
shangwe Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipowahutubia kwenye mkutano
huo.
Mgombea
wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimtambulisha mgombea
ubunge jimbo la ilombero Ndugu Abubakar Assenga almaarufu kama mtoto wa
fundi Cherehani kwenye mkutano wa kampeni za CCM zilizofanyika Ifakara
wilayani Kilombero.
Mgombea
wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa
Ifakara wilayani Kilombero kwenye mkutano wa kampeni za CCM ambapo
aliwaambia wananchi hao kuwa wakati wake utakuwa wa kiutendaji zaidi ili
kufanikisha maendeleo ya haraka kwa nchi na wananchi kwa jumla.
MGOMBEA
urais kwa tiketi ya CCM, Dk.John Magufuli amesema iwapo atachaguliwa
katika uchaguzi mkuu mwaka huu na kufanikiwa kuunda Serikali yake
atahakikisha baadhi ya mambo ya msingi atayaamua kwa kupata ushauri wa
marais waliomtangulia,amesema kuwa katika kipindi hiki cha kuomba ridhaa
ya wananchi ili awe Rais hatakuwa tayari kutoa matumani hewa ambayo
anajua wazi hayatekelezeki kwani ni dhambi na kufafafanua kila
anachoahidi anauhakika anao uwezo wa kutekeleza.
Akizungumza
kwenye mikutano yake mbalimbali ya kuomba ridhaa ya kuwania urais,
Dk.Magufuli aliwambia wananchi wa Ulanga kuwa anatambua dhamana
anayoomba kwa wananchi lakini ana uhakika malengo yake ya kuwatumikia
Watanzania na kuleta maendeleo yatafanikiwa kwani iwapo atahitaji
ushaauri ataupata kwa viongozi waliomtangulia kuongoza nchi.
Alisema
sifa kubwa ya Tanzania ni kwamba kuna viongozi wastaafu wengi wakimo
marais ambao wametanguli kuongoza nchi kuanzia awamu ya pili, ya tatu na
awamu ya nne.
“Iwapo
nahitaji ushauri, wapo viongozi wengi wa kunisaidia kuniongoza .Yupo
mzee Ali Hassan Mwinyi(Rais awamu ya pili), Rais mstaafu Benjamin Mkapa,
Rais Jakaya Kikwete,Rais mstaafu Salimn Amour na Rais mstaafu Aman
Abeid Karume.
“Huu ndio
utaratibu wan chi yetu kwamba wapo viongozi wa kutosha wa kunipa
ushauri katika kutekeleza majukumu yangu ya kuwatumikia Watanzania.Najua
msimamo wangu na Serikali nitakayoiunda ni kufanya kazi tu.Narudia tena
kwangu mimi ni kazi tu lakini bado ninao wazee wa kunishauri ili
nifikie malengo yangu,”alisema.
Alisema
kiongozi mzuri ni Yule ambaye anaweka malengo ya kuwatumikia wananchi
kwa misingi ya uzalendo na uadilifu na anapoona kuna mambo yanahitaji
ushauri kabla ya kufikia uamuzi wapo viongozi wa kumshauri na kumpa
mbinu za kufanya.
Dk.Magufuli
ameanza awamu ya pili ya kampeni baada ya kumaliza mikoa ya Nyanda za
Juu Kusini na Mkoa mmoja wa Kusini wa Mtwara ambapo jana ameanza ziara
Mkoa wa Morogoro.
Msafara
wa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha
Mapinduzi,Dkt John Pombe Magufuli ukikatiza kwenye dara la muda la Mto
Kilombero,ambalo hutumika kupitishia vifaa mbalimbali kwa ajili ya
ujenze wa daraja kubwa linalojengwa katika mto huo wa kilombero.
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi,Dkt
John Pombe Magufuli akikagua daraja la Mto kilombero ambalo ujenzi
wake unaendelea mpaka sasa.
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi,Dkt
John Pombe Magufuli akipata maelezo mafupi kuhusia na maendeleo ya
ujenzi wa dara hilo ambalo litakuwa mkombozi mkubwa kwa wakazi wa
Kilombero,litapunguza kero kubwa ya usafiri miongoni mwao kwa kiasi
kikibwa.
Baadhi ya
Viongozi wa Dini wakimwombea sala Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi,Dkt John Pombe Magufuli mara
baada ya kumaliza kuhutubia jioni ya leo kwenye mkutano wa kampeni
uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya msingi Mahenge jioni ya leo.
Mgombea
wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa
Ifakara wilayani Kilombero kwenye mkutano wa kampeni za CCM ambapo
aliwaambia wananchi hao kuwa wakati wake utakuwa wa kiutendaji zaidi ili
kufanikisha maendeleo ya haraka kwa nchi na wananchi kwa jumla.
Wanafuatilia kwa makini yaliyokuwa yakizungumzwa kwenye mkutano huo wa kampeni za CCM jioni ya leo mjini Ifakara
Mkutano wa kampeni za CCM ulipokuwa ukiendelea katika uwanja wa saba saba mjini Ifakara wilayani Kilombero jioni ya leo.
Mfuasi wa CCM na bango lake
Wananchi
wa mji wa Ifakara waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa kampeni za
CCM ndani ya uwanja wa saba saba wilayani Kilombero,wakimsikiliza kwa
makini mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipowahutubia kwenye mkutano
huo.
mgombea
ubunge jimbo la ilombero Ndugu Abubakar Assenga almaarufu kama mtoto wa
fundi Cherehani akizungumza jambo kwenye mkutano wa kampeni za CCM
zilizofanyika Ifakara wilayani Kilombero jioni ya leo.
Wananchi
wa mji wa Ifakara walaiojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa kampeni za
CCM ndani ya uwanja wa saba saba wilayani Kilombero,wakimsikiliza kwa
makini mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipowahutubia kwenye mkutano
huo.
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi,Dkt
John Pombe Magufuli akimkabidhi Ilani ya CCM Mgombea Udiwani wa CCM
wilaya ya Ulanga jioni ya leo kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika
kwenye uwanja wa shule ya msinfi Mahenge jioni ya leo.
Wananchi wakifuatilia hotuba ya Magufuli alipokuwa akipita kuwasalimia wananchi wa kijiji cha Lupiro-Ifakara wilayani Kilombero
nanchi wa
kijiji cha Lupiro-Ifakara wilayani Kilombero wakiwa wamefunga bara bara
wakimsimamisha Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia
chama cha Mapinduzi,Dkt John Pombe Magufuli awasalimie alipokuwa
akitokea Malinyi
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi,Dkt
John Pombe Magufuli akiwaaga wananchi wa mji wa Ifakara waliojitokeza
kwa wingi kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Saba
saba jioni ya leo.
Post a Comment