Picha zinatisha sana....Mlipuko waua watu zaidi ya 52...

Milipuko miwili imetokea wakati wa mkutano wa hadhara wenye lengo la maandamano ya amani katikati mwa Mji Mkuu wa Uturuki, Ankara asubuhi ya leo na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 52 na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa vibaya.

Picha za televisheni zilionyesha watu waliokuwa na hofu na wengine wakiwa wamelala chini wakiwa wametapakaa damu miilini mwao. 

Wakati duru ya pili ya uchaguzi wa ubunge ikitarajiwa kufanyika mwezi ujao, maandanmano hayo yalipangwa na vyama vya wafanyakazi wakitaka kumalizika kwa mashambulizi yanayoendeshwa na serikali dhidi ya wanamgambo wa Kikurdi.









Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top