TWIGA STARS YAAGA MICHUANO YA AFRIKA

TIMU ya soka ya wanawake ya Tanzania, Twiga Stars imetolewa katika hatua za Awali za Kombe la Mataifa ya Afrika, baada ya kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Zambia katika mchezo wa marudiano, Raundi ya Kwanza Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam jioni hii.
Matokeo hayo yanaifanya Zambia, Shepolopolo isonge mbele kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-2, kufuatia awali kushinda 2-1 nyumbani katika mchezo wa kwanza.


Twiga inayofundishwa na Rogasian Kaijage, iliuanza vizuri mchezo wa leo na kumaliza dakika 45 za kipindi cha kwanza ikiwa inaongoza bao 1-0, lililofungwa na Asha Rashid ‘Mwalala’ dakika ya 39.
Asha Mwalala alifunga akimalizia pasi ya Vumilia Maarifa, ambaye naye alipokea krosi ya Nahodha Sophia Mwasikili aliyewachambua wachezaji wa Zambia kwanza.
Kipa wa Twiga Stars, Fatuma Omary aliokoa mchomo wa hatari wa Mupopo Kabange dakika ya 75, lakini hakuweza kuuona mkwaju wa mpira wa adhabu uliopigwa na Rachel Ilungu dakika ya 80 kuipatia Zambia bao la kusawazisha.

Kikosi cha Tanzania kilikuwa; Fatuma Omary, Fatma Bashir, Deonisia Daniel, Fatma Issa, Evellyne Sekikubo, Sophia Mwasikili, Vumilia Maarifa, Amina Ali/Zena Khamis dk86, Asha Rashid, Shelda Boniface/Fatma Mustapha dk 65 na Eto Mlenzi.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top