MSHAMBULIAJI Olivier Giroud ametokea benchi na kufunga mabao mawili Arsenal ikiifunga Everton 4-1 na kujitengenezea mazingira ya kutinga Nusu Fainali za Kombe la Uwanja wa Wembley.
The Gunners walikuwa tayari mbele ndani ya dakika saba wakati Mesut Ozil alipojisafisha mbele ya mashabiki kwa kumtungua kipa wa Everton, Joel Robles.
Pamoja na hayo, Everton ikasawazisha kwa shambulizi la kushitukiza la Ross Barkley aliyempasia mfungaji Romelu Lukaku dakika ya 32.
Arsenal - ambayo inatakiwa kuifunga Bayern Munich wiki ijayo kukipiku kipigo cha 2-0 walichofungwa kwenye mechi ya kwanza ya Hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya, ilipata bao la kuongoza kupitia kwa kiungo wa zamani wa Everton, Mikel Arteta aliyefunga kwa penalti dakika ya 67. Giroud alifunga dakika ya 83 na 85 baada ya kuingia dakika ya 60 kuchukua nafasi ya Sanogo
Tumewanyamazisha: Olivier Giroud akimuinua Mesut Ozil juu baada ya kufungia Arsenal bao la nne
Giroud akifunga moja ya mabao yake leo
TUNAOMBA MAONI YAKO HAPA CHINI KUHUSU TAARIFA HII!!!
TUNAOMBA MAONI YAKO HAPA CHINI KUHUSU TAARIFA HII!!!
Post a Comment