Ajali mbaya ya gari Suye,barabara ya kuelekea Mjini Arusha mda mfupi uliopita......

 Ajali mbaya imetokea Mjini Arusha katika eneo la Suye, barabara ya kuelekea Moshono, Ajali hiyo imehusisha magari aina ya Hice "daladala" na Nissani Hard Body, na kupelekea Dereva wa daladala kuvunjika vibaya miguu yote miwili kutoka na magari hayo kugongana uso kwa uso.
Ajali hiyo imesababishwa na Dereva wa Nissani Hard Body ambaye alikuwa amelewa na kupelekea kuyumbayumba barabarani na hatimaye kuigonga daladala.
Katika Hali isiyo ya kawaida dereva wa Nissani Hard Body ambaye amesababisha ajali hiyo alipokua akijaribu kukimbia alitoa bastola kwaajili ya kuwatishia watu wasimzuie na ndipo kizaa kilipotokea na kusababisha barabara hiyo kufungwa kwa muda na kusababisha umati mkubwa wa watu kushuka kwenye magari na kulizunguka eneo hili.
Hata hivyo polisi waliweza kufika eneo hilo la tukio na kuweza kumdhibiti dereva wa gari aina ya Nissani Hard Body ambae amesababisha ajali hiyo na hatimaye hali ya utulivu imerejea.

Gari aina ya Nissan Hard Body ambayo namba zake yake ya usajili haikuweza kufahamika mara moja ikiwa imeharibika vibaya mara baada ya kusababisha ajali ya kugongana uso kwa uso na daladala katika eneo la Suye, Barabara ya kuelekea Moshono mjini Arusha muda mfupi uliopita.
  Daladala iliyogongana na Gari aina ya Nissani Hard Body muda mufi uliopita katika eneo la Suye barabara inayoelekea Moshono Mjini Arusha
  Daladala zilizogongana zikiwa zimetoka kabisa nje ya barabara mara baada ya ajali hiyo kutokea katika eneo la suye.
 Polisi wakiwa wamefika Eneo la tukio kwaajili ya kuhakikisha usalama na amani inakuwepo mara baada ya ajali hiyo kutokea.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top