Mzee ashushiwa kipigo cha kufa na raia wenye hasira kali.......Kisa Soma zaidi hapa

 Baba aliyetajwa kwa jina moja la Nuhu maarufu kama ‘Mzee Kijana’ (54), nusu auawe na raia wenye hasira kali, msimu wa Pasaka kisa kikiwa ni kuachiwa kwa dhamana isiyoeleweka baada ya kunaswa kwa kosa la ulawiti wa madenti.

Tukio hilo la kutisha lilijiri Aprili 19 (Ijumaa Kuu), mwaka huu maeneo ya Tuangoma-Mjimwema, Kigamboni jijini Dar,  mbele ya ofisi ya serikali ya mtaa huo ambapo awali, Aprili 9, mwaka huu ilidaiwa kuwa mzee huyo alidakwa na mmoja wa wazazi wa wanafunzi hao akiwa amemfungia kwa kufuli mwanaye ndani ya chumba chake huku mwenyewe akiwa katika shughuli zake za kuuza kuni.
Picha inaonyesha gari lililotumika kumchua mpaka kituoni.
Ilisemekana kwamba akiwa na mjumbe wa kitongoji hicho, mzazi huyo aliyepata fununu kuwa mwanaye wa kiume analawitiwa na mzee huyo, alifanya jitihada za kumsaka mzee huyo hadi kibaruani kwake ambapo alipohojiwa kama amemfungia mwanafunzi wake ndani ya chumba chake, mzee huyo alijiumauma na mwishoni kukubali.

Ilidaiwa kwamba wananchi na mzazi wa mwanafunzi huyo walimbeba mzee huyo msobemsobe hadi nyumbani kwake na kumtaka amfungue denti huyo ambapo alifanya kama alivyoagizwa kisha mwanafunzi huyo alichomolewa ndani ya chumba hicho.
Habari zilieleza kuwa sakata hilo lilitinga katika ofisi ya mtendaji ambapo walitoa taarifa kwa askari wa Kituo cha Polisi cha Kizuiani. Hata hivyo, ilisemekana kwamba askari hao walishindwa kufika kwa kuwa siku hiyo daraja la Kongowe lilikuwa limeharibika.
Ilisemekana kuwa baadaye walipata msaada kutoka kwa polisi wa Kituo cha Kibada, Kigamboni ambao walimchukua mtuhumiwa na baadaye kupelekwa Kizuiani kwa ajili ya taratibu za kisheria huku mwanafunzi huyo akipewa PF-3 kwa ajili ya uchunguzi kama kweli alikuwa akiingiliwa kinyume na maumbile.
Baadhi ya raia wenye hasira kali wakiwa nje ya kituo cha polisi alipofikishwa mtuhumiwa huyo.

Ilidaiwa kuwa kabla hata majibu ya daktari hayajachukuliwa, Mzee Kijana alionekana akirandaranda mitaani, jambo lililosababisha viongozi wa mtaa huo kuwasiliana na polisi kuhoji kulikoni?
Ilielezwa kuwa wakati wakuu hao wakihangaika na suala hilo ndipo wananchi wenye hasira kutoka kila upande waliivamia ofisi hiyo wakidai kuwa wamechoshwa na rushwa za wazi zinazofanywa na viongozi wao na kudai kuwa watampa adhabu mzee huyo wao wenyewe.
Ilidaiwa kwamba kufumba na kufumbua, watu hao wasio na idadi walivunja mlango na kumchomoa Mzee Kijana aliyekimbilia ofisini humo kwa ajili ya hifadhi na kuanza kumshambulia kwa kila aina ya silaha kiasi cha almanusura kumuua.
Kipigo hicho kilisababisha askari waliofika hapo ili kutuliza ghasia, kushindwa kazi, jambo lililowalazimu kutoka nduki ili kuokoa roho zao. Akizungumza na wanahabari wetu, mwenyekiti wa mtaa huo, Mohamed Chande alisema kuwa ilibidi aikimbie ofisi yake kwa kuwa watu walikuwa na ghadhabu kupita maelezo.
Inadaiwa kuwa msamaria mwema mmoja alimnyakua Mzee Kijana kutoka katika kundi la watu na kumpakiza kwenye gari lake haraka na kumsalimisha mikononi mwa Polisi wa Kizuiani ambapo inadaiwa kuwa hadi sasa yupo huko.
Akizungumza na waandishi wetu, bibi wa mwanafunzi huyo anayedaiwa kulawitiwa aliyejitambulisha kwa jina moja la Rugwesi (38), alisema kuwa alishangaa kuona mtuhumiwa akiachiwa kwa dhamana siku chache kabla hata majibu ya daktari hayajatoka.
“Ripoti imeonesha kuwa mjukuu wangu alikuwa akilawitiwa kwa muda mrefu na mzee huyo na si mjukuu wangu tu inadaiwa anawafanyia hivyo wanafunzi wengine watatu,” alisema bibi huyo huku simu ya mkuu wa Kituo cha Polisi Kizuiani ikiita bila kupokelewa.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top