MOTO WATEKETEZA MADUKA NA MGAHAWA MJINI DODOMA.......

Wananchi wa mji wa Dodoma wakiangalia sehemu ya madhara ya tukio la moto uliotokea usiku wa kuamkia leo katika baadhi ya maduka yaliopo kwenye Barabara ya Nyerere Karibu na Makao makuu ya CCM mjini Dodoma,moto huo umeteketeza maduka matatu na mgahawa wa New Chick Villa Reustaurant.
Maduka yaliyoathirika na moto huo ni Gulio La Mahafa Duka lililokuwa linauza bidhaa mbali mbali kwa jumla na reja reja zikiwamo bidhaa za Bakhresa,Duka la Esheki Investment lililo kuwa likiuza bidhaa za maofisini,vitabu na huduma ya uchapaji pomoja na Duka la madawa la lijulikanalo kama Kavula Pharmacy.Picha na Deusdedit Moshi,Globu ya Jamii Dodoma.Wakazi wa Mji wa Dodoma wakiendelea kuangalia maduka hayo huku wengi wao wakiwa hawaamini kilichotokea.Sehemu iliyokuwa na maduka ikiwa imeteketea kabisa kwa moto uliotokea leo Barabara ya Nyerere karibu na Ofisi za makao makuu ya Chama cha Mapinduzi CCM.





Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top