Kijana anayedhaniwa kuwa ni mwizi akipigwa na wananchi wenye hasira kaliKijana mmoja ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja amepigwa na kuumizwa na wananchi wenye hasira kali katika eneo la Msasani Bonde la mpunga jijini Dares salaam baada ya kugundulika kuwa ni mwizi.
Kijana akipakizwa kwenye pikipiki tayari kabisa kuelekea kituo cha polisi.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wamesema kwamba kijana huyo alijaribu kuiba pikipiki iliyopaki katika eneo la macho jijini Dares salaam, baada ya kushindwa kuiwasha alitokea mmiliki na kupiga mayowe ambapo watu walifurika na kuanza kumpiga.
Mwizi huyo alikimbilia katika dispensary ya Bonde la mpunga kujificha lakini haikufua dafu kwani watu wenye hasira walizingira dispensary na kumtoa nje kwa lengo la kumpiga. Lakini baada ya muda kidogo walifika askari wa jeshi la Polisi ambapo wamemchukua na kumpeleka kituo cha polisi cha Osta bay jijini Dares saam.
Wananchi wenye hasira wakimpiga kijana anayedhaniwa kuwa ni mwizi
Kijana anayedhaniwa kuwa ni mwizi
kijana huyo akiwa na majeraha mwilini kufuatia kupigwa na wananchi
Kijana akipelekwa katika kituo cha polisi
Dispensari ya Bonde la mpunga sehemu aliyokimbilia kijana huyo mwizi. Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote
Post a Comment