Lionel Messi apewa tuzo ya mchezaji bora na James Rodriguez ndiye mfungaji bora kombe la Dunia 2014

Licha ya kupoteza mechi ya fainali na kukosa kombe la dunia mwaka 2014, mshambuliaji wa Argentina na Barcelona, Lionel Messi ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa michuano ya kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil.

Tuzo hii imekuja katika hali ya kustaajabisha kwa watu wengi, lakini kwa kiasi kikubwa alistahili kupewa.

 Messi alionesha kiwango kikubwa katika hatua ya makundi akifunga mabao 4 katika michezo mitatu dhidi ya Bosnia, Iran na Nigeria, lakini nyota yake ilififia baada ya kushindwa kufunga katika mechi za mtoano dhidi ya Switzerland, Ubelgiji, Uholanzi na Ujerumani.
Katika mchezo wa fainali dhidi ya Ujerumani, Messi alipoteza nafasi moja muhimu, lakini muda mwingi alifanya jitihada za kutafuta upenyo bila mafanikio.

 Lionel Messi alipiga shuti, lakini alikosa bao katika mchezo wa fainali Maracana.

Baada ya kipyenga cha mwisho, Messi alipokea tuzo yake ya mchezaji bora akiwashinda  nyota wa Colombia James Rodriguez, winga wa Uholanzi, Arjen Robben na wachezaji watatu wa Ujerumani, Manuel Neuer, Bastian Schweinsteiger na Thomas Muller. 
Lionel Messi akiangalia chini baada ya kupoteza mechi ya fainali dhidi ya Ujerumani.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top