Ujerumani Mabingwa wa kombe la Dunia 2014....ushindi wa 1-0 kutoka kwa Mario Goetze..

Bao pekee la dakika ya 113 kupitia kwa kungo Mario Goetze limeiwezesha Ujerumani kutwaa ubingwa wa kombe la dunia 2014.

Argentina iliyocheza kwa kujihami zaidi, huku ikionekana wazi kusubiria hatua ya matuta, ikajikuta inalala 1-0 na kufanya historia ya fainali ya mwaka 1990 iliyozikutanisha timu hizo, ijirudie.

Kwa sehemu kubwa ya mchezo, Ujerumani walitandaza soka maridadi na kwa hakika imevuna ushindi iliostahili.
Uchawi wa Lionel Messi haukuweza kuisaidia lolote Argentina ambapo alidhibitiwa vizuri na safu ya ulinzi ya Ujerumani.

Kwa Messi na Muller kushindwa kufunga mchezo huu, mshambuliaji wa Colombia, James Rodriguez mwenye mabao sita, anakuwa ndiyo mfungaji bora wa kombe la dunia.
 Mabingwa 2014: Nahodha wa Ujerumani, Philipp Lahm (wa pili kulia mbele) akinyanyua kombe la dunia na kushangilia.
Wachezaji wa Ujerumani wakishangilia baada ya kutwaa kombe la dunia katika dimba la Maracana kwa kuifunga Argentina bao 1-0.
Big Bosi: Kocha wa Ujerumani, Joachim Low (katikati) akinyanyua Kombe la Dunia
 

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top