Upepo mkali uliovuma Zanzibar, Unguja waezua nyumba na kuharibu mazingira

 Upepo uliovuma  kwa dakika  kumi katika eneo la pongwe wilaya ya kati  mkoa wa kusini unguja umeezua paa za nyumba 11, kung'oa miti  na kusababisha uharibifu wa mazingira .

Akitoa taarifa  kamanda wa polisi mkoa wa kusini Unguja SACP kamishna msaiidzi Juma Saad Khamis amemsmea upepo mkali ulitokea mchana na ulikuwa waghafla  kiasi cha kuwachanganya  wakaazi wa eneo hilo la Pongwe pwani   na kusababisha hasara  kubwa kwa familia za wananchi hao.
Nae mkazi wa eneo hilo Said Juma Nyange ameelezea jinsi upepo huo ulivokuja na kuharibu mali za wanaanchi huku Sheha huyo akielzea hatua zinazochukuliwa na hasara zilzopatokea.

Hata hivyo wakati upepo huo umeleta hasara kubwa hapakuwepo  na taarifa yeyote ya tahadhari au onyo lolote kwa wanaanchi wa mkoa huo kutoka mamlaka ya hali ya hewa  afisi ya Zanzibar  kuijiandaa na upepo huo.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top