Kadi ya raisi wa Marekani Barack Obama yakataliwa

Rais wa Marekani Barack Obama amejikuta katika wakati mgumu baada ya kadi yake ya muamana (credit card) kukataliwa katika mojawapo ya migahawa iliyopo jijini New York.Obama amekiri kukutana na mkasa huo alipokuwa akizunguma na waandishi wa habari baada ya kusaini agizo la rais litakalotumika kama sheria ya matumizi ya kadi za muamana ambayo itasaidia katika kuzuia wizi wa kadi hizo ambao umekithiri nchini humo.
Akizungumzia mkasa wa kukataliwa kadi yake, Obama amesema alifika katika mgahawa mmoja na baada ya kuhudumiwa vitafunwa, mara baada ya kadi kuingizwa katika mashine iligoma kufanya muamana, ndipo alipohisi kuwa kuna namna kadi hizo ‘zinachakachuliwa’, hivyo akalazimika kutumia kadi ya mkewe Michelle Obama kufanya muamana huo.
Tatizo la wizi wa kadi za muamana limeathiri watu takribani milioni 100 kwa mwaka jana, ambapo kusainiwa kwa agizo hilo la rais wa Marekani kutasaidia katika kuhakikisha usalama wa huduma za muamana na pia kuanzishwa kwa huduma ya dharura mtandaoni itakayowahudumia watumiaji waliopoteza kadi zao.
Marekani ni moja ya nchi zinazotoa huduma za kadi ya muamana ambapo mtumiaji wa huduma hiyo anakuwa na uwezo wa kupata huduma za malipo ya baada kwa manunuzi ya bidhaa na huduma mbali mbali.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top