Lowassa awaasa wananchi kujitokesa siku ya kupiga kura ili wampate kiongozi muadilifu

EDWARD Lowassa, mgombea urais wa Chadema amesema, Rais Jakaya Kikwete ameharibu uchumi wa Tanzania.

Akizungumza na wafuasi wa Chadema pia UKAWA katika ofisi za Chadema mara baada ya kuchukua fomu ya kuwania urais kupitia chama hicho jana mchana, Lowassa  alisema;

“Rafiki yangu Jakaya Kikwete ameuharibu uchumi wa nchi yetu,”

“Wakati Rais Mkapa anaondoka madarakani kilo ya sukari ilikuwa Sh. 600 leo ni Sh. 2,300. Mchele ulikuwa Sh. 550 leo ni Sh. 2,300. Sembe ilikuwa Sh. 250 leo ni Sh. 1,200.”
 

Aidha Lowassa alisema, katika kipindi cha utawala wa Rais Kikwete ndipo Tembo na kila aina ya wanyama wameuwawa kuliko kipindi chochote katika historia ya Tanzania.

“Katika utawala wa Rais Kikwete, Tembo wameuwawa kuliko kipindi chochote katika historia duniani kote.

“Kila aina ya mnyama ameuwawa kuliko kipindi chochote katika historia ya nchi yetu. Nitaijenga serikali yenye uchumi kwa speed (kasi), ambaye hawezi akae pembeni,” alisema Lowassa  na  kuongeza:

"Nauchukia sana umaskini kama ugonjwa wa ukoma, dhamira yangu ni kwenda Ikulu ili kupambana nao kwa nguvu na akili zangu zote...katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu, asilimia 72 ya vijana ndio watakaopiga kura hivyo naenda Ikulu kutengeneza Serikali.
"Serikali yangu itakuwa rafiki kwa waendesha pikipiki za bodaboda, mamalishe na wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama wamachinga hivyo tunzeni vichinjio vya kupigia kura (vitambulisho).

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top