Polisi wakamata mabomu Mkoani Kagera

Jeshi la polisi mkoani Kagera limefanikiwa kukamata mabomu manne ya kutupwa kwa mikono na Magazini mbili zilizokuwa na jumla ya risasi mioamoja hamsini kutoka kwa majambazi walikuwa wamejiandaa kufanya matukio ya uharifu katika  kituo kidogo cha Polisi Kalenge kilichopo wilayani Biharamulo.
Akithibisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa jeshi la Polisi mkoani Kagera Agustine Ollomi amesema majambazi hao walikuwa wakitokea wilayani Kibondo mkoani kigoma wakieleka wilayani kahama ambapo jeshi hillo  liweka mtego wake na majambazi hao walifanikiwa lukimbia kusiko julikana na na kuacha silaha hizo pamoja na mabomu manne waliyokuwa wakitaka  kufanyia uharifu ambapo walikimbia kusikojulikana nakwamba jeshi la  polisi linaendelea na msako wakuwatafuta majambazi hao.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani kagera amesema kwa sasa jeshi la polisi linaendelea kuimarisha ulinzi wakutosha na kuhakikisha linadhibiti matukio ya ujamabazi wa kutumia silaha za moto hasa katika kipindi hiki gumu cha kuelekea uchaguzi mkuu.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top