JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA.
“PRESS RELEASE” TAREHE 03.09.2015.
· MTU MMOJA AFARIKI BAADA YA KUGONGWA NA GARI WILAYA YA MBARALI.
· MPANDA BAISKELI AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI WILAYA YA MBOZI.
· WATU SITA WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA BAADA YA KUFANYIKA OPERESHENI.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTU
MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA BOKA KASULA (50) MKAZI WA SONYANGA
AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI YENYE NAMBA ZA USAJILI ALP
3965 AINA YA SCANIA BASI MALI YA KAMPUNI YA WADACHOVU
ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA DEREVA ERNEST CLEMENCE (42) MKAZI WA ILOMBA
IKITOKEA DSM KUELEKEA MALAWI.
AJALI
HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE 02.09.2015 MAJIRA YA SAA 23:00 USIKU HUKO
KATIKA KIJIJI CHA SONYANGA, KATA YA MAHONGOLE, TARAFA YA ILONGO, WILAYA
YA MBARALI, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA KUU YA MBEYA/NJOMBE.
MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KITUO CHA AFYA IGURUSI. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI, DEREVA AMEKAMATWA. UPELELEZI UNAENDELEA.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MPANDA
BAISKELI ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA THADEO MWASHILANGA (21) MKAZI WA
ICHENJEZYA WILAYA YA MBOZI AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI
ISIYOFAHAMIKA.
AJALI
HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE 02.09.2015 MAJIRA YA SAA 06:00 ASUBUHI HUKO
KATIKA KIJIJI CHA ILOLO, KATA YA MLOWO, TARAFA YA VWAWA, WILAYA YA
MBOZI, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA KUU YA MBEYA/TUNDUMA.
MWILI
WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA WILAYA YA MBOZI. CHANZO NI MWENDO
KASI NA DEREVA ALIKIMBIA NA GARI BAADA YA TUKIO. UPELELEZI UNAENDELEA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z.
MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO
IKIWA NI PAMOJA NA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI
KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
TAARIFA ZA MISAKO:
MTU
MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA AIDAN JOHN (32) MKAZI WA UYOLE-MBEYA
ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA BHANGI UZITO
WA GRAM 25.
MTUHUMIWA
ALIKAMATWA KATIKA OPERESHENI ILIYOFANYIKA MNAMO TAREHE
02.09.2015 MAJIRA YA SAA 15:30 JIONI HUKO KATIKA KITONGOJI CHA
KAMFICHENI, KIJIJI NA KATA YA MKWAJUNI, MKWAJUNI, TARAFA YA KWIMBA,
WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA.
KATIKA OPERESHENI ILIYOFANYIKA
MNAMO TAREHE 02.09.2015 MAJIRA YA SAA 12:00 MCHANA HUKO ENEO LA
MATENKI, KATA YA NJISI, TARAFA YA UNYAKYUSA, WILAYA YA KYELA, MKOA WA
MBEYA, MTU MMOJA AITWAYE MWINUKA NGONYA (30) MKAZI WA MATENKI AKIWA NA
POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU NCHINI AINA YA RIDDER BOKSI
08 NA CHARGER BOKSI 2.
AIDHA
KATIKA OPERESHENI ILIYOFANYIKA WILAYANI CHUNYA MNAMO TAREHE
02.09.2015 MAJIRA YA SAA 15:30 JIONI HUKO KATIKA KIJIJI CHA MATUNDASI
[B], KATA YA MATUNDASI, TARAFA YA KIWANJA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA
MBEYA, WATU WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA GEORGE SAWELA (44) MKAZI
WA MATUNDASI NA GILBERT SILWANI (43) MKAZI WA MATUNDASI WAKIWA NA
MILIPUKO BARUTI 136 PINI ZA MILIPUKO 35, COTEX MITA 70 NA DOTNETOR
2 BILA KIBALI.
TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI WATUHUMIWA MARA BAADA YA UPELELEZI KUKAMILIKA ZINAENDELEA.
Imetolewa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Post a Comment