Wastara na Bond kufunga ndoa baada ya Uchaguzi

SASA imethibitika kuwa ndoa kati ya muigizaji nyota wa filamu Wastara Juma na Mtangazaji Bond Suleiman itafanyika mara baada ya uchaguzi mkuu ujao.

Bond ambaye pia ni muigizaji, aliongea na tovuti hii kuwa wawili hao wameshafikia muafaka wa kuoana lakini Wastara yupo bize na kampeni, kwani baada ya kuanguka katika ubunge wa viti maalum kwa tiketi ya CCM, sasa anazunguka mikoani na Samia Suluhu ambaye ni mgombea mwenza wa John Magufuli jambo ambalo limesababisha washindwe kufanya maandalizi.

“Unajua Wastara amejiingiza kwenye siasa na mimi nataka akomae kwani itakuja kutusaidia baadaye ndiyo maana tumekubaliana kuahirisha ndoa mpaka uchaguzi uishe ndipo tutapanga tena,” alisema

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top