Makosa yakuyaepuka unapoandika barua ya kuomba kazi..

Wengi  wanaotafuta kazi wameonekana kupuuzia kuandika barua za kikazi kwa kuamini kuwa “ CV” zao ndo muhimu hilo ni kosa kubwa sana na wengi wamepoteza nafasi ya kwa njia hiyo.Hapa Blog yako ya Amewezaje kwa utafiti wa muda mrefu inakuonesha makosa ambayo wengi wanayafanya katika kuandika barua za maombi ya kazi..

1.Kutuma barua yenye makosa madogomadogo.mfano makosa ya kisarufi na herufi hii ni tatizo kubwa kwani mwajiri anaona wewe hauko makini hivyo barua yako utupiliwa mbali.Pitia barua yako kabla hujaituma.

2.Kutuma barua ya jumla(barua moja inatumwa  kwa watu waajiri wengi bila kurekebishwa)Hakikisha unataja kazi unayoomba kwenye sentensi ya kwanza.Elezea uzoefu wako na ujuzi wako kulingana na nafasi husika.

3.Barua kutokwenda kwa mhusika.Wengi wa wanaoomba kazi wametokea kutuma barua kwa mtu ambaye si sahihi hii ni kutokana na kutuma maombi mengi ya kazi.Hakikisha unapitia mawasiliano yako kabla hujatuma kwa mhusika.

4.Kutumia salamu zilizopitwa na wakati.Wengi hutumia salamu za zamani sana kama vile “Dear Sir or Madam” Unaweza tumia “Dear Human Resource Manager”Kama unamfahamu waweza  andika jina lake mfano kwa mwanamke tumia “Ms. Rachel” badala ya “Mrs Rachel”

5. Barua kuwa fupi sana.Barua kuwa fupi ni hali itayopelekea mwajiri kuona kuwa nia yako  ni ndogo sana katika kazi.Pia hutashindwa kueleza uzoefu wako na historia katika kazi ulokuwa ukifanya na hivyo huwezi kumshawishi mwajiri kwa lolote.

6.Barua kuwa ndefu sana.Barua ikiwa ndefu zaidi inawezakuwa mzigo kwa msomaji na inamshawishi kuiacha na kusoma za watu wengine.Hakuna haja ya kuwa na aya nyingi katika barua aya 3 hadi 5 zinatosha sana na zisiwe na mistari zaidi ya 6.

7.Kuandika barua yenye maelezo mengi yasiyo lazima.Kuna taarifa ambazo si za kundikwa kwenye barua,unatakiwa kuandika taarifa zinazohitajika katika nafasi husika kwa mwajiri.Barua ikiwa ndefu itakupunguzia uwezekano wakuchaguliwa katika usaili.

8.Kutokutoa mifano halisi.Kueleza mawazo matupu kuhusu uwezo wako pasipo mifano ya majukumu ulofanya ambayo yamekupatia uwezo huo ni kazi bure na huwezi kumshawishi mwajiri.Taja mifano hai na majukumu ulokuwa ukifanya yalokupa ujuzi mfano ninauwezo mkubwa wa mauzo kwani kwa kipindi nilichofanya kazi katika kampuni x nimewezesha kampuni kuuza mara tatu ya mauzo ya kawaida.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top