Moto wateketeza gari ndogo aina ya land cruzer

Taharuki imewakumba wakazi wa mji wa kibondo mkoani Kigoma baada ya gari dogo aina ya land cruzer kuungua moto huku kukiwa amna jitihada zozote za kuzima moto moto huo kutokana na wilaya hiyo kutokuwa na huduma ya magari ya zimamoto.

Gari hiyo aina ya toyota land cruzer iliyokuwa imebeba tanki dogo la mafuta nyuma lilishika moto na dereva kulazimika kulikimbia gari lake katika eneo la wazi huku likiendelea kuwaka na hivyo kusaidia kutoleta madhara makubwa kwa jamii, ambapo wananchi kutokana na tukio hilo wameiomba serikali kuweka huduma za zima moto na kuzingatia sheria juu ya ubebaji wa mafuta au matanki ya mafuta yanayoweza kusababisha mlipuko.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya kibondo Luis Bura amesema wilaya hiyo imeweka mikakati wa kutoa elimu na kuhakikisha kila mahali panapohitaji kuwepo vifaa vya zimamoto vinakuwepo ambapo ameliagiza jeshi la polis kuwachukulia hatua wananchi wanaokaidi kutii sheria za zimamoto..


Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top