Magufuli aahidi kurejesha imani ya CCM

Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli amesema kazi ya kwanza atakayoifanya ni kurejesha imani ya chama hicho kwa wananchi kwa maelezo kuwa kilianza kupoteza dira na kuwa chama cha matajiri.

Akizungumza katika hafla fupi ya kumkaribisha kwa mara ya kwanza jijini Dar es Salaam kama mwenyekiti wa CCM,  Magufuli alisema waliokuwa wakitafuta fedha za miradi na majengo ya chama hicho watafute pa kutokea.

Alisema chama hicho kimejipanga kujisahihisha na kuanzia sasa wasio na fedha ndani ya chama hicho ruksa kugombea uongozi.

Huku akitolea mfano jinsi alivyojitosa kuwania urais bila kuwa na chochote,  alisema chini ya uongozi wake hakuna kigogo ndani ya chama hicho atakayekwenda kinyume na taratibu na akapona.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top