TBS yakifungia kiwanda cha mikate

Shirika la viwango Tanzania, TBS limekifungia kiwanda kimoja cha kutengeneza mikate cha jijini Dar es Salaam kutokana na kuzalisha mikate bila kuthibitishwa ubora wake na shirika hilo.

Zoezi hilo lilianza jijini Dar ambapo shirika hilo la viwango limekibaini kiwanda cha Heri bakery kilichopo Kiwalani na kufungwa kwa muda usiojulikana.

Afisa Mthibiti Ubora mwandamizi TBS, Zainabu Mziray alisema, “Kwa kawaida ni kwamba wazalishaji wote wanapaswa kuwa na nembo ya ubora ili kuhakikisha walaji chakula wanachokula ni chenye ubora unaotakiwa, kwahiyo hawa hawana nembo ya ubora na hawajafanya hatua zozote za kupata nembo ya ubora”, alisema.

Aliongeza kuwa kusema, “licha ya kukosa vyeti vinavyoonesha uhalali wa kuzalisha mikate hiyo kutoka TBS, hawana vyeti vya aina hiyo kutoka katika taasisi nyingine za serikali, jambo linalothibitisha kuwa wamekuwa wakifanya uzalishaji wa mikate hiyo ilimradi na kuhatarisha afya za walaji,” aliongeza.

Bi Mziray alidai kuwa walianza kampeni hiyo tangu Januari na watakuwa wakienda kwenye viwanda na kupita katika masoko kutambua vitu visivyo na ubora kwa kushtukiza ili waweze kutambua vitu visivyo na ubora.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top