Apigwa risasi 27 na watu wasiojulikana na kupoteza maisha

Usiku wa kuamkia march 19 ,2014 kumetokea tukio la kusikitisha baada ya kijana Luiz Carlos mwenye umri wa miaka 25 kupoteza maisha baada ya kupigwa risasi  27 na watu waliojitambulisha kuwa ni maafisa wa polisi wakati anatoka nyumbani kwake Iguacu-Brazil.

Uchunguzi wa polisi unaonyesha kuwa watu hao waliojitambulisha kuwa ni maafisa wa polisi walikuwa ni majambazi  na baada ya kijana huyo kuwagundua ndipo watu hao walipoanza  kumpiga risasi tumboni ambazo zilipelekea utumbo wake kutoka nje na vilevile walimpiga risasi ya mguu na ya kifua.

Wahalifu hao baada ya kumpiga risasi  kijana Luiz na kuona utumbo wake ukining'inia nje walidhani kwamba alikuwa tayari amekufa hila haiukuwa hivyo kwani ilimchukua muda kupoteza maisha na hata alipoulizwa na polisi juu ya tukio hilo hakuweza kusema chochote hadi alipopoteza maisha.
Kwa mujibu wa kamishna Mpelelezi wa makosa ya jinai bwana Wichnecki alisema haiwezekani watu waue pasipo kuwa na sababu inawezekana wanachanzo na hivyo upelelezi utaendelea ili kuweza kutambua chanzo cha tukio hilo.
 Kwa mujibu wa baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo  walidai kuwa siku zote "mtu atakae uwa kwa upanga basi nae atauawa kwa upanga".




Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top