Mchezo wa masumbwi Aprili 26 Muddy Matumla kuzipiga na Fransic Miyeyusho

Mabondia Fransic Miyeyusho 'Chichi Mawe' na Mohamed Matumla 'Snake JR' wamesaini mkataba wa kupambana april 26. Akizungumzia mpambano huo promota wa mchezo wa masumbwi nchini Ally Mwazoa amesema ameingia nao mkataba mabondia hawo kwa kuwa anajua wanaweza mchezo wa masumbwi na ni mafundi wa mchezo huo najua kuna watu wengi walitamani kudhamini mchezo huo lakini bahati imeniangukia kwangu, mpambano huu utakaopigwa april 26 katika ukumbi wa PTA sabasaba ambapo kutakuwa kutakuwa na mapambano mengine makali ya utangulizi,Mwana dada Lulu Kayage atamvaana na Halima Ramadhani siku hiyo kwa ajili ya kuhamasisha wanawake wenzao wajitokeze katika mchezo wa masumbwi.
Promota Ally Mwazoa katikati akiwatambulisha mabondia Fransic Miyeyusho kushoto na Mohamed Matumla wakati wa kutangaza mpambano wao utakaofanyika April 26 katika ukumbi wa PTA Sabasaba.
Bondia Fransic Miyeyusho wakitunishiana misuli na Mohamed Matumla wakati wa utambulisho wa mpambano.

Baada ya kusaini mkataba huu bondia Miyeyusho alijitamba kuendeleza ubabe katika familia hiyo ambapo alisema atamchakaza kama alivyo mchakaza baba yake mdogo Mbwana Matumla ambaye amecheza nae mara tatu na kupigwa mara mbili ambapo mpambano wa mwisho ulikuwa na shamu shamu nyingi kila upande miyeyeyusho alibuka mshindi kwa point.

Matumla alijibu mapigo kwa kusema Miyeyusho anamuheshimu kwa kuwa yeye ni mkubwa kiumri ata hivyo atampa kichapo kikali kama alivyompatia mdogo wake Doi Miyeyusho ambaye mara ya kwaza alipigwa kwa K,O raundi ya pili DDC Keko na mara ya pili pia K,O ya raundi ya pili katika ukumbi uho uho wa PTA Sabasaba hivyo siwezi kushusha rekodi yangu kwa kupigwa na miyeyusho akitaka kujua mimi ni mkali zaidi yao amulize pia Nassibu Ramadhani ambaye nilimpatia kipigo kibaya sana na kunifanya ninyakue pikipiki.
 Bondia Fransic Miyeyusho kushoto na Mohamed Matumla wakikumbatiana baada ya kukubaliana kuzipiga April 26 katika ukumbi wa PTA Sabasaba.
 
Mwazoa aliongeza kuwa ulizi na usalama wa mali zako ni wa huwakika hivyo familia nzima mnaweza kuja kushudia mpambano huo wa masumbwi bila shaka. 
Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile:-
Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi.
Pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha mchezo huu wa masumbwi hapa nchini.


TUNAOMBA MAONI YAKO HAPA CHINI KUHUSU TAARIFA HII!!! 

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top