Man United mechi ya tatu hakuna ushindi yalazimishwa sare 0-0 na Burnley

Kocha wa zamani wa Manchester United, Sir Alex Ferguson akiwa na David Gill na Sir Bobby Charlton wakitazama mchezo wa timu hiyo ikilazimishwa sare ya 0-0 na Burnley.

United imekuwa ikisuasua tangu kustaafu kwa Ferguson mwaka jana. Makocha wawili wamekwishapewa timu, David Moyes aliyetimuliwa mwishoni mwa msimu uliopita na Ryan Giggs akakaimu kumalizia msimu, kabla ya msimu huu kuajiriwa Louis Van Gaal ambaye amefikisha mechi ya tatu bila ushindi, sare mbili ugenini, nyingine 1-1 na Sunderland na kufungwa moja nyumbani na Swansea City 2-1.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top