Man City yakubali kipigo cha kwanza msimu huu toka kwa Stoke city

Manchester City wamepunguzwa kasi katika Ligi Kuu ya England baada ya kukubali kipigo cha kwanza msimu huu kutoka kwa Stoke City 1-0 Uwanja wa Etihad jana jioni.

Alikuwa ni Mame Biram Diouf aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 58, baada ya mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester United kuwatoka mabeki wa City na kumaliza uteja wa kufungwa mechi sita mfululizo Etihad.
Diouf akishangilia baada ya kuifungia bao pekee Stoke City Uwanja wa Etihad
Kikosi cha Man City kilikuwa:
Hart, Sagna, Kompany, Demichelis, Kolarov, Silva, Fernando/Fernandinho dk38, Toure, Nasri/Navas dk63, Jovetic/Dzeko dk63 na Aguero.
Kikosi cha Stoke city kilikuwa:
Begovic, Bardsley, Shawcross, Wilson, Pieters, Walters/Odemwingie dk45, Adam, Whelan, Nzonzi, Moses/Muniesa dk80, Crouch na Diouf.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top