Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar linamshikilia Afisa Usalama Feki aliyekamatwa na silaha

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia mtu mmoja anayefahamika kwa jina la Gunner Meena (40) mkazi wa Kinyerezi, Segerea, Dar es Salaam,  kwa tuhuma za kujifanya  mtumishi wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Tukio la mwisho lililomfanya akamatwe ni pale alipomtishia mfanyabiashara mwenye asili ya Kisomali aitwaye Abdi Dalmar, ili ampe Tshs 25,000,000/= ama sivyo angechukua hatua chini ya Sheria ya Usalama wa Taifa.

Aidha jeshi hilo katika kuendesha oparesheni zake za kutokomeza ujambazi wa kutumia silaha limefanikiwa kukamata  bastola nne na shot-gun moja wiki hii.
Baadhi ya silaha zilizokamatwa na jeshi la polisi.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top