BREAKING NEWS: Bunge maalumu la katiba lapitisha Rasimu ya Katiba leo Bungeni Dodoma!

Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samuel Sitta hivi punde ametangaza rasmi kupitisha Rasimu ya Katiba inayopendekezwa baada ya matokeo kutangazwa.‎


Hatua hiyo imefikiwa baada ya kura za ndio zilizopigwa na wajumbe kufikia kiwango kinachostahili.
Ili katiba hiyo iliyopendekezwa ipite ilitakiwa kuungwa mkono na kura za ndio theluthi mbili kutoka Tanzania bara na theluthi mbili za ndio kutoka Zanzibar.

Jumla ya wajumbe wote wa bunge hilo la Katiba ni 629, huku 419 wakitoka Tanzania bara na 210 kutoka Zanzibar.

1. ZANZIBAR.

* Sura ya Kwanza Ibara ya 1 hadi 11 imepata theluthi Mbili

* Sura ya Pili Ibara ya Ibara ya 12 hadi 21 imepata theluthi mbili

* Sura ya Tatu Ibara ya 22 hadi 22 hadi26 imepata theluthi mbili

* Sura ya Nne Ibara ya 27 hadi 30 imepata theluthi mbili

* Sura ya Tano Ibara ya 31 hadi 64 imepata theluthi mbil

*Sura ya Sita Ibara ya 65 hadi 69 imepata theluthi mbili

*Sura ya Saba Ibara ya 70 hadi 75 imepata theluthi mbili

*Sura ya nane Ibara ya 76 hadi 121 imepata theluthi mbili

*Sura ya Tisa Ibara ya 122 hadi 123 imepata theluthi mbili

*Sura ya Kumi Inara ya 124 hadi 157 imepata theluthi mbili

*Sura ya Kumi na Moja Ibara ya 158 hadi 161 imepata theluthi mbili

*Sura ya Kumi na Mbili Ibara ya 162 hadi 202 imepata theluthi mbili

*Sura ya Kumi na Tatu Ibara ya 203 hadi 208 A imepata theluthi mbili

*Sura ya Kumi na Nne Ibara ya 209 hadi 221 imepata theluthi mbili

*Sura ya Kumi na Tano Ibara ya 222 hadi 242 A. imepata theluthi mbili

*Sura ya Kumi na Sita Ibara ya 243 hadi 257. imepata theluthi mbili

*Sura ya Kumi na Saba Ibara ya 258 hadi 269. imepata theluthi mbili

*Sura ya Kumi na Nane Ibara ya 270 hadi 274. imepata theluthi mbili

*Sura ya Kumi na Tisa Ibara ya 275 hadi 289. imepata theluthi mbili


Zoezi hilo la upigaji kura ambalo lilianza Septemba 29 mpaka Oktoba 2, siku matokeo yalipotangazwa, lilisusiwa na wabunge wengi wa upinzani, kwa madai kuwa baadhi ya vipengele vya awali vilivyopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyopewa kazi ya kukusanya maoni kutoka kwa mwananchi, vilikuwa vimeondolewa.

Kabla ya kupitishwa kwa rasimu hiyo, bunge hilo maalum la katiba lilikaa kama kamati kujadili mapendekezo katika Rasimu ya Katiba iliyoandaliwa na tume hiyo ya Mabadiliko ya Katiba iliyokuwa chini ya uongozi wa Jaji Joseph Warioba.

Baada ya kamati hizo za bunge hilo kutoa mapendekezo yao, kamati ya uandishi ilikuwa na jukumu la kuandika upya Ibara za Sura za Rasimu ya Katiba zilizojadiliwa na Bunge Maalum na hatimaye kutoa taarifa kwa Mwenyekiti baada ya kukamilisha kazi hiyo.

Hivyo, Kamati ya Uandishi ilikuwa na jukumu la kuhakikisha kuwa mapendekezo ya marekebisho, maboresho au mabadiliko katika Rasimu ya Katiba yanakidhi matakwa na masharti ya Kanuni za Bunge Maalum za Mwaka 2014.

Hatma ya katiba hiyo itahitimishwa kwa kura ya maoni inayotarajiwa kupigwa na wananchi.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top