Kitoto kichanga chaokotwa dampo Makorora Mkoani Tanga.

Kitoto kichanga kinachokadiriwa kuwa na umri wa siku mbili kimeokotwa kikiwa kimefariki katika dampo lisilo Rasmi lililopo katika eneo la kwa king'afu Makorora jijini Tanga kikiwa kimenyofolewa baadhi ya viungo vyake vya mwili kuashiria kuwa kilitupwa baada ya mama yake mzazi kujifungua.
Baadhi ya watu waliokuwa wakipita katika eneo hilo jirani na barabara kuu inayounganisha mitaa ya makorora,sahare,mabanda ya papa na gatundu kuhisi baadhi ya kunguru wakinyemelea mwili wa marehemu ndipo waliposogea karibu na kuona mwili huo ambapo baadhi ya watu hasa akina mama walikemea vikali kitendo hicho cha mauaji.

Kwa Upande wake Mkuu wa kituo kinacholea watoto waliotupwa katika Mazingira kama hayo kinachojulikana kwa jina la ''Nyumba ya Furaha'' Sister Joyce Mdemu amekemea kitendo hicho cha mauaji kwa sababu kama mtuhumiwa ameshindwa kukilea kichanga hicho cha umri wa siku mbili ni vyema angechukua maamuzi ya kukipeleka katika kituo maalum chakulelea watoto wa aina hiyo kwa sababu huenda kichanga hicho ndicho kingekuwa kiongozi wa taifa la kesho.

Kwaupande wao baadhi ya watoto waliotupwa na kutelekezwa kama kilivyokuwa kichanga hicho wakielezea mafanikio baada ya kuokolewa kisha kulelewa na kituoni hapo tangu wakiwa wachanga na baadae kuanza shule hadi sekondari wamewataka wasamaria wema kuwaaidia watoto waliotupwa na kuokotwa wakiwa hai pamoja na kuelekeza misaada yao kwa wale wanaoishi katika mazingira hatarishi mitaani kwa kuwapeleka shule kwa sababu hao ndio taifa la kesho.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top