James Mbatia awataka watanzania wasifanye makosa

Mwenyekiti wa chama cha NCCR mageuzi James Mbatia amewataka wananchi  wasifanye makosa wachague viongozi waadilifu wenye  hofu ya mungu na wenye uwezo wa kupigania maslahi mapana ya taifa kwa faida za wengi.

Mbatia ameyasema hayo  wakati akizungumza kwenye mkutano wa wanawake katika  viwanja vya makuyuni himo ambapo amesema  huu sio wakati wa kubahatisha na kuwataka wanawake walililie taifa hili kuhakikisha wanachagua viongozi wenye msukumo wa kubadilisha maisha ya watanzania walio wengi kazi ambayo amesema Mh,.Edward Lowasa anaiweza.

Katibu mkuu wa baraza la wanawake wa chama cha demokrasia na maendeleo  Grace Tendega akizungumza  kwenye mkutano huo amesema wanwake wamekuwa wakitumika kama madaraja ya kuvusha watu kisiasa lakini amewataka mwaka huu wafanye mabadiliko washiriki kikamilifu kuchagua viongozi ambayo watatengeneza serikali itakayosimamaia vipaumbele vya wanwake na watoto.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top