Magufuli aahidi kumaliza mapigano ya wakulima na wafugaji, Dodoma

Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia umati wa watu kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma jana.

Akitoa hotuba yake katika mji wa Kibaigwa Dk. John Pombe Magufuli alisema hakuna kitu kinachomuumiza kama mauaji ya wakulima na wafugaji yanayotokea kati ya wilaya za Kongwa Mkoani Dodoma na Kiteto mkoani Manyara.

Dkt Magufuli aliahidi kuwa mara baada ya kuchaguliwa na kuunda Serikali yake, jambo hilo atalipa uzito wa juu na kulifanyia kazi kwa umakini mkubwa.

“Yaani mimi Magufuli nimteuwe Waziri na watendaji wengine wa serikali halafu mauaji yatokee watu wafe, Mkuu wa mkoa yupo, Mkuu wa wilaya yupo na Kamanda wa Polisi yupo wabaki wanapunga upepo... wamiliki wa ng’ombe wabaki wanakula maisha... haiwezekani! Nitalala nao mbele na ng’ombe wataliwa msibani kwa uzembe waliousababisha” alisema Magufuli kwa msisitizo mkubwa.

Magufuli amewataka wafugaji na wakulima kuishi kwa amani bila kubaguana, lakini pia akasema atatumia sheria za ardhi na kuhakikisha maeneo ya wafugaji na wakulima yanatengwa, ili wafanye shughuli zao na kukuza kipato na uchumi wao bila kusumbuliwa.
Waziri Mkuu wa zamani, Jaji Mstaafu Joseph Warioba, akimnadi Dkt.Magufuli kwa kuhubiri amani katika mikitano yake ya kampeni kuliko wagombea wa vyama vingine hawasisitizi kudumisha amani nchini jambo ambalo ni tunu ya taiafa
Dkt. Magufuli akimnadi mgombea Ubunge wa Dodoma Mjini,mara baada ya kumkabidhi Ilani ya Uchaguzi ya CCM, Ndugu Anthony Mavunde wakati wa mkutano wa kampeni kwenye Uwanja wa Jamhuri mjni Dodoma leo.
Dk Magufuli akimnadi Mgombea ubunge Jimbo la Mpwapwa, George Lubeleje,mjini MPwapwa katika uwanja wa mgambo.
Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akimnadi Mgombea ubunge Jimbo la Kongwa, Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai wakati wa mkutano wa kampeni jimboni humo.
Mawaziri wakuu wa zamani, John Samuel Malecela na Jaji Mstaafu Joseph Sinde Warioba wakifuatilia mkutano wa kampeni wa Dkt Magufuli alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Dodoma kwenye mkutano wa kampeni.
Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli, akimsimamia Mgombea ubunge Jimbo la Mtera kupitia CCM, Livingstone Lusinde aliyekuwa akifanya mazoezi ya Push Up wakati wa mkutano wa kampeni kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa akimuombea kura Dk Magufuli wakati wa mkutano huo wa kampeni mjini Dodoma  jana jioni .
Walemavu nao wana haki ya kuwasikiliza wagombea nafasi mbalimbali ikiwemo ya Urais,Ubunge na Udiwani
Wananchi wa Kibaigwa wilayani Kongwa, wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM,Dkt. Magufuli alipokuwa akiwahutubia katika mkutano wa kampeni mjini Kongwa.
Mgombea Urais Dkt John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Waziri Mkuu wa zamani Jaji Mstaafu Joseph Sinde Warioba,mjini Kibaigwa wilayani Kongwa kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
Wananchi wa Kibaigwa wilayani Kongwa wakifuatilia hotuba za Dkt Magufuli kwenye mkutano wa kampeni.
Dk Magufuli akijipigia kampeni kwa wakazi wa Kibaigwa , wilayani Kongwa jana.
Dkt. Magufuli akiwapungia mikono wananchi alipowasili kwenye kampeni Uwanja wa Jamhuri Dodoma jana.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top