Breaking news: Mchungaji Christopher Mtikila afariki dunia katika ajali

Habari zilizotufikia hivi punde ni kwamba mwenyekiti wa Chama cha DP nchini Tanzania mchungaji Christopher Mtikila amefariki dunia asubuhi hii Majira ya saa 12 kasorobo katika ajali katika Kijiji cha Msolwa karibu na mji wa Chalinze takribani kilomita 15 hivi kutoka Chalinze barabara ya Morogoro mkoani Pwani

Kamanda wa polisi mkoa wa Pwani Jafar Ibrahim amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba watu wengine watatu waliokuwa katika gari hilo wamekimbizwa hospitali kwa ajili ya matibabu.

"Kwa maelezo ya dereva,gari ndogo aina ya Salon waliyokuwa wanasafiria iliacha njia wakiwa wanaelekea jijini Dar es salaam,ikapinduka,ilikuwa na watu wanne akiwemo dereva na mchungaji Mtikila,hawa watatu ni majeruhi na mchungaji Mtikila inasemekana amefariki,mwili wa marehemu na majeruhi wako njia wakielekea hospitali ya Tumbi",amesema Kamanda Ibrahim.

Amesema bado wanachunguza chanzo cha ajali hiyo...


Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top