Baba wa Diamond Platinumz afunguka mazito kuhusu Mtoto wake

Baba mzazi wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Abdul Jumaa amekuwa akisema mengi mazito juu ya mwanaye huyo lakini safari hii ni kama ‘yamemfika hapa’ kufuatia kauli yake kwamba, siku akifa staa huyo asimzike, Ijumaa limezungumza naye kwa takriban dakika 45.

Akizungumza kwa njia ya simu huku akionekana kutokuwa na matumaini ya mwanaye huyo kumsamehe, Mzee Abdul alieleza kuwa amefikia hatua ya kusema hayo kutokana na ukweli kwamba haoni faida ya kuwa na mtoto anayeitwa Diamond.

“Kwa anayonifanyia ni vyema ajihesabie tu kwamba hana baba, amenidhalilisha sana, sasa kama ameshindwa kunijali na kunisaidia nikiwa hai, nikifa kutakuwa na faida gani kuja kunizika?” alihoji mzee huyo.
 
KUMBE SIYO DIAMOND TU
Mzee huyo ambaye kwa sasa afya yake si nzuri akisumbuliwa na miguu bila msaada wowote wa kimatibabu aliendelea kusema kuwa, siyo Diamond tu kwani hata mwanaye mwingine, Mwajuma Abdul ‘Queen Darleen’ ambaye naye ni msanii wa Bongo Fleva ameungana na kaka yake.

“Sioni faida ya watoto hawa ambao hawana msaada kwangu, hata Mwajuma (Queen Darleen) tangu apewe gari na kaka yake amezidi kunitupa, hivyo bora nikae nikijua sina watoto kuliko kuwa na watoto mastaa halafu hawana msaada kwangu.

“Kwa hiyo nasema nimechoka kabisa, sioni faida ya mtu kuja kunizika nitakapokufa wakati nipo hai hanijali, hakuna kitu kinachoniumiza kama pale ninaposikia Diamond anasaidia watu baki wakati mimi baba yake nateseka.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top