Vijana wakipata joto ya jiwe baada ya kukutwa mchana wa Ramadhaan Machomanne Chake Pemba wakifanya mambo kinyume na maadili ya mwezi mtukufu.
Elimu bado inahitajika kwa waumini kuweza kufahamu na kuelimishwa kuhusiana na funga kwani licha ya kuwa ni amri kutoka kwa Allaah Subhaanahu Wata'ala pia ni moja katika nguzo kuu tano za dini ya kiislamu.

Kula kwa makusudi au kufanya jambo litakalobatilisha funga kwa makusudi mchana wa Ramadhaan si kwamba kunabatilisha funga tu bali kunaweza kukutoa katika dini pia kwa mujibu wa baadhi ya Maulamaa kwa kuikana moja katika nguzo za kiislamu.
Tusichoke kuwakumbusha ndugu umuhimu wa kujitambua na kujielewa kwamba ni Waislamu na tutaulizwa na Muumba siku ya siku
Tusichoke kuwakumbusha ndugu umuhimu wa kujitambua na kujielewa kwamba ni Waislamu na tutaulizwa na Muumba siku ya siku
2 comments
Siafikiani na wewe hata kwa asilimia 2! swala la dini ni mapokeo na inahusisha imani ya mtu, hailazimishwi! acha mtu aamini vile anavyo amini! na ndio sababu kuna uhuru wa kuabudu!
ReplyNi kweli ulichokisema lakin hiyo imetokea kama njia moja wapo ya kuwakumbusha baadhi ya vijana wanojisahau kuhusu maadili ya Dini ya kiislamu
ReplyPost a Comment