Watu 17 wamefariki dunia kwenye ajali ya barabarani baada ya basi la kampuni ya MoroBest lililokuwa likitokea wilayani mpwapwa mkoa wa Dodoma kwenda jijini Dar es salaam kugongana uso kwa uso na lori lilikuwa limesheheni mabomba ya maji likitokea morogoro kwenda dodoma katika eneo la pandambili wilayani kongwa huku zaidi ya watu 45 wakijeruhiwa.
Paparaziwetu alifika eneo la tukio na kushuhudia basi hilo lenye namba za usajili T258 AHV aina ya Scania pamoja na lori lenye namba za usajili T820 CQU likiwa na tela lenye namba T390 CKT yakiwa yameharibika vibaya ambapo kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo wanasema ilitokea wakati lori likijaribu kulipita lori lingine na likiwa kwenye mwendo wa kasi na mbele yake lilitokea basi na dereva wa lori akashindwa kulimudu na kugongana uso kwa uso.
Mara baada ya kutokea ajali hiyo maofisa wa jeshi la polisi kutoka mkoa wa Dodoma na wilaya ya Kongwa pamoja na baadhi ya viongozi wa serikali akiwemo mkuu wa wilaya ya Mpwapwa ambapo basi hilo lilitokea na kaimu mkurugenzi wa wilaya ya Kongwa walikuwa wakisimamia shughuli za uokoaji na hapa wanaeleza hatua za awali zilizochukuliwa.
Nje ya hosipitali ya rufaa ya Dodoma magari ya wagonjwa yanamiminika kuleta majeruhi wa ajali hiyo ambapo baadhi ya majeruhi wanazungumzia ajali hiyo huku mganga mkuu wa mkoa wa Dodoma Ezekiel Mpuya akithibitisha kupokea majeruhi 22 hosipitalini hapo huku majeruhi wengine 20 wakipelekwa hosipitali ya wilaya ya Kongwa.
Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma David Misime anathibitisha kutokea kwa ajali hiyo huku jeshi la polisi likiendelea kufanya uchunguzi wa kitaalamu kujua nini chanzo na kiini cha ajali hiyo.
Baadhi ya Miili ya Marehemu muda mchache baada ya ajali hiyo
Baadhi ya wasamaria wema wakiwa wanaendelea kuokoa majeruhi na kuwaondoa waliofariki
Hivi ndivyo basi lilivyo Haribika
Endelea kuwa nanasi hapa hapa kwa habari na matukio zaidi....
Post a Comment