Mtu mmoja afariki dunia na wengine sita kujeruhiwa mkoani Morogoro baada ya kuangukiwa na Lori la kokoto

Mtu mmoja  amefariki dunia papo hapo na wengine sita wamejeruhiwa baada ya kuangukiwa na lori lilisheheni kokoto waakati likijaribu kukwepa mwendesha pikipiki kisha kuacha njia na kupinduka na kuwaangukia watembea na kuwabana kwa masaa kadhaa katika eneo la msamvu mjini Morogoro.

Vilio na mazonzi vilitawala katika eneo la tukio la ajali wakati zoezi la kuokoa mtu aliebanwa na gari likiendelea ambapo kamanda polisi mkoa wa Morogoro Lenarld Paul akizungumza katika eneo la tukio  amesema chanzo cha ajali ni uzembe wa derva wa pikipiki aliekatisha barabarani bila utaratibu ndipo lori hilo aina ya isuzu liliacha njia na kuwaangukia watembea kwa miguu. 
Baadhi ya mashuhudua wa tukio hilo akiwemo mbunge wa jimbo la Morogoro mjini Mh Abdulaziz Abdood  ameomba serikali kufikiria  upya kuweka matuta katika barabara hiyo ili kupunguza ajali zisizokuwa za lazima huku wananchi wakilalamikia ukosefu wa vitendea kazi vya uokoaji nao baadhi ya wafanyakazi wa kiwnada cha kutengeneza nguo za michezo cha Mazava wamesema waliojeruhiwa ni wafanyakzi wenzao na walikua wakitokea kazini ambapo  wamelalamikia msongamano wa wafanyakazi  wanapotoka kiwandani hulazimika kutumia geti moja linalotokea katika barabara kuu ya Morogoro Iringa.

Katika hospitali ya mkoa wa Morogoro walikolazwa majeruhi muuguzi wa zamu Merad Jackson amekiri kupokea maiti na majeruhi na hali za wagonjwa mmoja bado hali yake ni mbaya na wote wanaendelea na matibabu.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top