NI kweli ajali haina kinga! Nyota wa nyimbo za Injili Bongo, Bahati Lusako Bukuku ameumia mgongo na maeneo kadhaa ya mwili kiasi cha kushindwa kukaa, kusimama wala kutembea kufuatia ajali mbaya ya gari iliyotokea kwenye eneo la Ranchi ya Narco wilayani Kongwa, Dodoma saa tisa usiku wa kuamkia Jumamosi, Ijumaa Wikienda lina undani wa mkasa mzima.
Kwa mujibu wa chanzo makini, katika ajali hiyo ambayo Bahati alikuwa akienda Kahama, Shinyanga kwenye mkutano wa Injili, dereva wa gari alilokuwa akisafiria aina ya Toyota Nadia lenye namba za usajili IT 7945, Edison Mwakabungu ‘Eddy’ (31) aliumia sana kwenye vidole vya miguu na hawezi kutembea.
Kwa mujibu wa chanzo makini, katika ajali hiyo ambayo Bahati alikuwa akienda Kahama, Shinyanga kwenye mkutano wa Injili, dereva wa gari alilokuwa akisafiria aina ya Toyota Nadia lenye namba za usajili IT 7945, Edison Mwakabungu ‘Eddy’ (31) aliumia sana kwenye vidole vya miguu na hawezi kutembea.
Wengine waliokuwemo kwenye ajali hiyo ni wacheza shoo wa Bahati, Frank Muha (20) na mwenzake ambaye jina lake halikupatikana mara moja.
Habari zilidai kuwa gari hilo halikuwa na matatizo hivyo kumfanya dereva wake kukanyaga mafuta kwa wastani wa kilometa 120 kwa saa.“Sasa walipofika eneo la Kibaigwa, walikutana na lori likitokea Dodoma kwenda Morogoro, wakavaana kwa mbele. Nadia likatoka barabarani hadi porini likiwa limeharibika kuanzia kwenye shoo ya mbele, injini na siti za mbele halafu lori hilo likakimbia.
“Nadia ilipotulia, Bahati alijikuta hawezi kufanya chochote, dereva wake naye ameumia kwenye vidole vya miguu. Wale wawili waliokuwa siti ya nyuma, wote walijeruhiwa lakini mmoja si sana. Ilibidi yeye abaki pale na gari ili majeruhi wengine wakimbizwe Hospitali ya Wilaya ya Kongwa, Dodoma kwa matibabu,” kilisema chanzo hicho.
Habari ambazo hazijathibitishwa na dereva wa Bahati zilisema kuwa, wakati gari hilo linakaribiana na lori, dereva wa lori aliwasha taa ‘full’ (mwanga mkali) hivyo kumfanya dereva huyo kushindwa kuona mbele vizuri, jambo ambalo ni kinyume na sheria za usalama barabarani.
Alfajiri ya juzi,paparaziwetu alimpigia simu Bahati na kuongea naye kuhusu ajali hiyo ambapo huku akisikika kama anayepata tabu kwa maumivu, alisema:
“Ni kweli tumepata ajali, nimeumia mgongoni, dereva ameumia mguu. Namshukuru Mungu. Sijui nini kilitokea, nilishtukia kuona gari kubwa mbele yetu likituvaa, mara nikashtukia tuko porini. Lakini kabla ya safari Dar tulifanya maombi makubwa, najua Mungu ametunusuru na kifo kibaya,” alisema Bahati.
Paparaziwetu alipojaribu kumuoji: “Unadhani nani alikuwa na kosa kati ya dereva wako na wa lori?”Bahati: “Sijui chochote. Halafu najisikia vibaya sana, tuwasiliane baadaye kaka ‘angu.”
Habari zinasema kwamba, Eddy ni dereva wa miaka mingi. Mbali na jijini Dar, pia amekuwa akiendesha magari kwenda nje ya Tanzania kama Burundi na Rwanda na katika ajali hiyo alikuwa akienda nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC), hivyo ana uzoefu wa safari za usiku.
Kumbukumbu zinaonesha kuwa hii si mara ya kwanza kuripotiwa kwa ajali za magari mkoani Dodoma zikiwahusisha watu wa tasnia Injili Bongo.
Endelea kuungana nasi katika paparaziwetu.blogspot.com kwa habari na matukio ya kila siku ndani na nje ya tanzania yetu
Post a Comment