Diamond asema yupo tayari kushirikiana na Ali Kiba

Kama ulikuwa unawasiwasi kuwa haitawahi kutokea collabo ya Diamond na msanii mwenzake ambaye alikuwa akitajwa kuwa na tofauti nae Alikiba, sasa unaweza kupunguza mashaka sababu Diamond yupo tayari kuingia booth na mwimbaji huyo wa ‘Mwana’ endapo atatakiwa kufanya hivyo (lakini endapo kama na Alikiba atakuwa tayari kwa ofa hiyo).
Diamond Platnumz amesema yupo tayari kufanya collabo na Alikiba au msanii yeyote atakayehitaji msaada wake. 
“Mimi sina tatizo, inategemea ni project gani inategemea ni muziki gani kwasababu nimeshawasaidia watu wengi nimefanya nao macollabo kwanini mtu anavyokuja nifanye nae collabo yeye nikatae, yaani siwezi kukataa” Diamond ameiambia 255 ya XXL ya Clouds Fm.
“mwaka huu kwanza zitatoka nyimbo nyingi za macollabo ambayo wasanii wengi wa Nigeria nimewasaidia nimefanya nao nyimbo, wengi sana. Kcee nimefanya nae, nimefanya na Mafikizolo, nimefanya na yule Waje, nimefanya na Don Jazzy, nimefanya na Dr Sid, nimesaidia watu wengi sana. Kwahiyo kama naweza kufanya wa huko kwanini nisifanye na mtu wa nyumbani, nikishindwa kufanya na mtu wa nyumbani nitakuwa na roho mbaya, au nitakuwa sitaki kusaidia kwasababu namshukuru mwenyezi Mungu muziki wangu kidogo umefika hatua sio mbaya, so nikifanya na mtu wa nyumbani na yeye namfikisha katika hatua ambayo hajawahi kufika bado, so mi siwezi kumkatalia mtu yeyote”.

Ni hivi karibuni tu msanii Wizkid wa Nigeria nae alipoulizwa swali kama hilo kama ikitokea akatakiwa kufanya collabo na mpinzani wake Davido, nae alisema kila kitu kinawezekana.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top