Everton wapigwa 6-3 na Chelsea...... Matokeo ya mechi zote za Jana Jumamosi haya hapa

Chelsea imezidi kugawa kipigo Ligi Kuu ya England baada ya kuifumua Everton kwa bao 6-3.Ilikuwa ni mechi ya aina yake ya funga ni kufunge, lakini mwisho wa siku timu makini yenye wachezaji makini ikaibuka kuwa mshindi.
Mshambuliaji mpya wa Chelsea Diego Costa ameendelea kucheka na nyavu katika kila mechi.Costa akatupia wavuni mabao mawili, goli la kwanza likiwa limetinga dakika ya kwanza ya mchezo na bao la mwisho alilofunga dakika ya 90. Magoli mengine ya Chelsea yalifungwa na Branislav Ivanovic dakika ya 3, goli la kujifunga la Seamus Coleman dakika ya 67 na Nemanja Matic dakika ya 74.

Everton walipata magoli yao kupitia kwa Kevin Mirallas dakika ya 45, Steven Naismith dakika ya 69 na Samuel Eto’o dakika ya 76.

Kikosi cha Everton kilikuwa:

Howard, Coleman, Jagielka, Distin, Baines, McCarthy, Barry, Mirallas, Naismith, McGeady (Eto'o 70), Lukaku (Besic 89).

Kikosi cha Chelsea:

Courtois, Ivanovic, Cahill, Terry, Azpilicueta, Ramires, Matic,Willian (Mikel 75),Fabregas (Drogba 89),Hazard (Luis 83), Costa.

Matokeo ya mechi zote za Ligi Kuu zilizochezwa Jana Jumamosi ni:
                  Burnley           0 - 0  Manchester United 
 
Manchester City       0 - 1   Stoke City

           Newcastle United 3 - 3   Crystal Palace
 
Queens Park Rangers 1 - 0   Sunderland
       
  
                        Swansea City 3 - 0 West Bromwich Albion

         West Ham United  1 - 3   Southampton

       Everton          3 - 6   Chelsea

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top