Jeshi la Polisi Wilaya ya Chalinze mkoani Pwani, linafanya kazi zake kwenye kontena mali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kutokana na ufinyu wa majengo ya ofisi.
Hayo yalisemwa mjini Chalinze jana na Diwani wa Bwilingu, Nasa Karama wakati wa makabidhiano ya kompyuta na sh milioni 11 za kusaidia ujenzi wa vituo vya polisi msaada uliotolewa na Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete.
Karama alimueleza mbunge huyo kuwa tangu kituo hicho cha polisi kipandishwe hadhi kuwa cha wilaya, shughuli zimeongezeka hali iliyoilazimu CCM kuruhusu kontena lake litumike kama sehemu ya ofisi za kituo hicho.

Alisema askari wa kituo hicho hawana nyumba za kuishi, wamepanga uraiani hivyo alimuomba Ridhiwani kusaidia ujenzi wa nyumba za askari polisi hao.
Akikabidhi misaada hiyo kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Ulrich Matei mbunge huyo alisema kompyuta na mashine ya kudurufu nyaraka zitasaidia kuhifadhi kumbukumbu na kuacha matumizi ya steshenari za nje ya ofisi.
Akishukuru baada ya kukabidhiwa misaada hiyo, Kamanda Matei alisema kituo cha Chalinze kimepandishwa hadhi ni kipya hivyo kinahitaji maboresho.

Post a Comment